Tuesday, March 8, 2011

Mchungaji Ambilikile na Fursa ya Utalii wa Tiba Tanzania

KAMA Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76) angezuka kwenye nchi kama Italia au Spain au Bahama auBarbados au hata Kenya au Botswana au Afrika Kusini au Seychelles hapa Afrika, nadhani serikali katika nchi hizozingelijikusuru ndani ya muda mfupi tu kujenga mazingira ambayo yangeliwezesha tiba kuendelea na wananchi wa Kijiji cha Samunge, Sale, wilayani Ngorongoro kulala maskini na kuamka tajiri. Na wakati huo mkoa wa Arusha na nchi nzima kunufaika kiuchumi na kimatangazo duniani kwa bei sawa na bure.


Tunaposema serikali ijitoe katika kuendesha masuala ya uchumi hatuna maana ijiondoe pia hata katika ubunifu, kupanda mbegu, kustawisha na kukuza vitu kama hivi. Kufanya hivyo ninaamini ni makosa, tena makubwa sana. Na ni kuwatendea isivyo haki wananchi. Maana kama tunaweza kuwaachia watu wakachota fedha za EPA, lakini tunashindwa kutumia vijisenti vichache vya serikali kujenga miundombinu na kutoa huduma muhimu huko Samunge basi upo walakini mkubwa kiuongozi!


Inavyoelekea kama kawaida yetu sera na watendaji wetu serikalini hawana utambuzi wala hawajachangamka na kuitambua fursa ya
'mgeni aje mwenyeji apone.'


Kwa maneno mengine kama serikali ya mkoa wa Arusha na serikali kuu zikiweza kukisaidia kijiji hicho kwa hali na mali katika masuala muhimu ya miundo mbinu na huduma za dharura umaskini katika eneo hilo unaweza ukafutika ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu.


Pengine kwa kuwa hao wanaotegemewa kuyafanya mambo hayo nao wamo katika misafara ya kuelekea huko huko Loliondo. Lakini ninaamini hata kama wasingelikwenda huko mambo yangelikuwa vivi hivi. Basi makala hii pia itumike kuwashtua angalau wale watakaokuwa na busara na hekima baada ya kwenda kuaguliwa huko warudi wanakorudi, wajipange na wafanye kile kinachohitjika ili baraka iliyojileta yenyewe isijegeuka baa au balaa ya mwaka.


Utalii kwa Watanzania walio wengi una maana ya kwenda kuona wanyama na vivutio vilivyozoeleka nchini. Lakini kuna utalii wa aina nyingi. Kuna utalii wa mambo ya kale au historia na kumbukumbu, utamaduni, michezo mbalimbali midodgo kwa mikubwa, mbio za magari, farasi,pikipiki na baiskeli, starehe, kamari, kuogelea na kulala ufukweni, kuwinda, kutembelea maeneo yenye maajabu nchini na mali asili.


Aina mpya za utalii zinazojitokeza sasa ni pamoja na utalii wa vijijini (watalii kuishi na kuwasaidia watu vijijini, jamii (wanajamii wenyewe kumiliki mahoteli, magari na biashara zingine za kitalii), elimu (wanafunzi na walimu kuja kuishi kwa muda nchini), utafiti na utoaji huduma maalum ikiwemo tiba asili, mbadala na ile ya miujiza.


Kwa yakini kila binadamu anachokifanya kikawa tofauti au adimu na nadra kuonekana kwingine huwa nacho ni kivutio cha utalii. Kwa maneno mengine, binadamu kutokana na akili aliyopewa na Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kutengeneza pia vivutio vipya vya utalii. Safari hii lakini Mwenyezi Mungu ameamua kukitengeneza mwenyewe kivutio kwa kupitia Mchungaji Ambilikile. HIvi dunia itatuona vipi kama tumepewa kivutio kama hiki halafu tukakosa akili na dhamira ya kunufaika nacho ?


Kilichotokea Arusha baada ya Mchungaji Ambilikile kuanza kuponesha watu kimiujiza ni fursa ambayo haijawahi tena kujitokeza Tanzania. Ni fursa ya papo kwa papo kujenga na kunufaika na utalii wa tiba inayotolewa kwa karama aliyopewa Mchungaji Ambikile.


Huko Ureno na Hispania ambako kuna mawaziri na watendaji wa sekta ya utalii ambao kila wakilala, wakila, wakiamka na wakitembea huwaza kitu kimoja tu-jinsi ya kupata fursa mpya za kukuza utalii nchini kwao, mambo haya yalishatokea na hivi leo maeneo husika ni mojawapo ya vivutio vikuu vya utalii katika nchi zao.


Kama tunavyochangamkia kutuma FFU wakati wa maandamano haya au yale, hii ilikuwa ni nafasi ya mwaka kutuma jeshi la wananchi na vikosi vya mangimeza kwenda kuhakikisha barabara zinatengenezwa; mahema yanawekwa; maboza ya maji yanapeleka maji kila kukichwa; mama ntilie wanapewa usafiri wa bure kwenda kuanzisha biashara ya muda; pia bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wagonjwa watarajiwa na wageni wengine watakavyohitaji vinapelekwa ili kufanya biashara. Hili lingeweza kufanywa kwa ubia kati ya serikali ya mkoa na wananchi wa huko wakisaidiwa na serikali kuu na vyombo vyake.


Ukiona watu wako tayari kutumia vyombo vya dola kuharibu na kulemaza rasilimali muhimu kuliko zote katika nchi, yaani watu, badala ya kuvifanya vyombo hivyo kutoa mchango chanya katika maendeleo ya jamii na kiuchumi ni lazima ujiulize maswali mengi.


Na hata wale wenye uroho na uchu mkubwa wa vyeo na madaraka ambao wamo katika mkoa husika wanaposhindwa kuliona hili nao wakaingilia kuimba wimbo wa mbwa-mwitu, mbwa mwitu wa mchungaji wa Esopo badala ya ule wa Ambilikile jua hamna kitu hapo ndugu.


Wananchi wa Kijiji cha Samunge, kama Tanzania ingelikuwa na Benki na taasisi kama hizozinazoona mbali na mbele na zinazojali maendeelo ya kweli ya Watanzania wangelipewa mikopo chapuchapu kuongeza vyumba viwili-vitatu kwenye nyumba/viwanja vyao ili nao wanufaike kwa kupangisha vyumba hivyo kwa wageni na kutoa huduma za chakula na kadhalika.


Benki zingelisaidia pia upatikanaji wa maji, umeme na huduma mbalimbali zinazohitajika na watu wanaokwenda kutafuta tiba Semunge.


Tumewaona wanasiasa wakipeperushwa na helikopta huku na kule, lakini kwa kuwa tumeshakubali kuwa Watanzania wasiokuwa viongozi ni walaniwa wa kupanda mabasi yaendayo kwa fujo, treni mbovu na meli chakavu hakuna aliyewaza kuwa ujio wa Mchungaji Ambilikile nao unahitaji pia kuwe na kiwanja cha helikopta kama sio cha ndege karibu na pale anakotoa dawa. Kwa kuwa watu wamemuamini na wanapona nina hakika nauli ya kupanda helikopta kutoka Arusha hadi Semunge isingeliwashinda watu.


Lakini kinachotokea sasa ni kwamba kwa kuwa hakuna anayefikiria haya, basi jamaa zetu kama kawaida wametafuta njia ya mkato ma rahisi kama walivyozoea. Njia hiyo siyo nyingine, ila ni kuzuia wagonjwa wasielekeee Loliondo kwa muda.


Watu waliokata tamaa na ghafla kuwa na matumaini mapya ya kupona sasa wamewekwa njia panda. Wako njia panda kwa sababu wale wanaosimamia mambo yao wameshindwa kuitambua fursa hii ya kuwa na utalii wa Tiba huko Semunge, Ngorongoro.


Utalii ambao tukiuchangamkia mapato yake kwa sasa yakitoka mfukoni mwa Watanzania yangeweza kabisa kuzidi mara kadhaa mapato ya utalii yanayotokana na watalii kutoka nje hapo wilayaniNgorongoro.


Ni mambo kama haya yanaonesha tofauti kati ya serikali yenye watu wasiolala nawanaowaza saa zote juu ya maendeleo ya watu na serikali ambayo viongozi wake wamelala na wako madarakani kujishughulisha na uchungaji kondoo wa mali zao na wanapozinduliwa toka usingizini huanza kupiga mayowe ya mbwa mwitu, mbwa mwitu!


Ninaamini, huu ndio mwanzo. Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, Warundi, Wakongomani, Wazambia na Wamalawi wako njiani. Isitoshe watu toka Uarabuni, Uchina, Ulaya na Marekani nao watakuja.


Kama tunakubaliana juu ya hilo hapo juu basi ni vyema watendaji wa serikali na hususan wanaobeba dhima ya kuujenga na kuuendeleza utalii nchini waamke. Wakishaamka, wahahe huku na huku kutafuta misaada toka kwa taasisi na watu husika ili kuona kama mawazo yangu ya Ki-Alinacha yanaweza kufanyiwa kazi.
Siwezi kushangaa kama ghafla nchi jirani zitaanza kuomba ruhusa ya kuingiza helikopta zenye wagonjwa Semunge. Hii itakuwa ni baraka na neema, lakini pia aibu ya mwaka kwa watendaji wetu nchini!


Na serikali inapashwa kuonesha njia katika hili. Vinginevyo itajikuta inapiga ngoma isiyo na wachezaji, maana watu wote wanakimbilia kwa manju wapya!

Sunday, March 6, 2011

Uongozi, Ukiritimba na Rasilimali za Maendeleo

UDIKTETA au ukiritimba kwa mtu mmoja kuhodhi mamlaka yote peke yake, iwe kisiasa au kiuchumi au kijamii huashiria kuwpo mtu au kikundi cha watu wasiojiamini na wasiokuwa na uhakika wa kile wanaschostahili wanachokifanya. Aghalabu watu wa namna hii huwa hawajui wanakotoka wala wanakokwenda. Kihistoria na kimustakabali ni muflisi. Ni mwanzo wa ufichaji maovu mengi kwa kuonesha mazuri machache ambayo pengine hayana manufaa kwa binadamu. Udikteta una tabia ya kuwageuza watu wote wajinga, mazezeta na wakorofi na wachache walioko madarakani kuwa ndio watu bora, wanaojua kila kitu wastaarabu na wazalendo wa kweli. Hata hivyo, jambo hili pia huwa na tabia ya kujichimbia kaburi lake yenyewe. Huanza kwa kutoamini wengine lakini huishia kwa kutojiamini wenyewe na kutoaminiana wenyewe kwa wenyewe na kuishia kwa wao wenyewe kujichanganya na kujimaliza.
Udikteta huweza kuundwa na mtu mmoja au kikundi cha watu. Udikteta uliopo Tanzania hivi leo ni ule wa kichama. Udikteta unaokifanya chama kimoja kujiona kimeokoka na kitakatifu zaidi kuliko vyama vingine. Eti peke yake na wanasiasa wake tu ndio wanaoweza kufanya mema na mazuri kwa nchi. Udikteta unaotaka kuwaaminisha watu eti kwamba chama kinachotawala peke yake ndicho kinachotaka kudumisha amani, umoja na mshikamano nchini na vyama vingine ni hatari na tishio kwa umoja na amani yetu. Jambo ambalo si kweli bali unafiki na danganya toto ya wale wanaotaka kula nchi bila kubughudhiwa. Na haya tumeyaona huko Tunisia, Misri na yakingali yanaendelea Libya, Bahrain, Oman, Yemen na kadhalika.

Udikteta huu unajidhirisha kwa chama hicho kutaka kuwa na watu na sauti katika kila jambo hata yale yasiyokihusu- kwa mfano, dini, utamaduni, mila na desturi, mawasiliano, maendeleo ya watu na jamii zao, ushirika, uzalishaji mali na majumuiko mengine ya kijamii kwa hofu hii au ile.
Katika miaka hii kila mkoa utakuwa ukijiuliza sisi kama mkoa tunapata NINI, tunapata toka kwa NANI, tunakipata LINI, tunapata kwa ajili ya NANI na KWANINI tunapata kitu tunachopata HIVI SASA, ni NANI anayetupa, yuko WAPI, NA ANATUPA KWA SABABU gani na kwa NAMNA GANI ILI YEYE NA SISI TUPATE nini kwa ajili ya nini NA KINA NANI ? Na tunachopewa ni SAMAKI au ni NDOANA au nyavu za sisi wenyewe KUVUA?

Na je kwa mpango huu tutapata maendeleo baada ya miaka michache au baada ya miongo kama sio karne? Maana wakishaingia madarakani viongozi wa Kiafrika hudhani wananchi wameuimbwa kuwa wavumilivu hata katika yale mambo yanayopaswa kutekelezwa ndani ya juma au mwezi tu! Ili mradi wao wanaishi na kula vizuri, wanapanda helikopta na ndege na hakuna wanachokosa msamiati wenye maneno kama haraka na dharura kwao hamna. Uvumilivu kama huo utakuwa ni vigumu kupatikana huko tunakokwenda.
Kwa kuwa wanasiasa waliopo wanaamini hawawezi kuitawala nchi bila ya kulazimisha mikoa, wilaya, vijiji na mitaa kuwa chini ya chama tawala basi miundo, kanuni na mifumo ya kisiasa inayoundwa sio ile ya kufanya maeneo hayo kuwa huru bali maeneo hayo kutawaliwa moja kwa moja au kimzunguko na chama tawala na viongozi wake.
Ni dhahiri basi madaraka mikoani au kuwa na mikoa huru kiuchumi na kijamii sio jambo linaloweza kufanywa na wanasiasa wa chama tawala. Hili ni jambo linalostahili kuwemo kwenye katiba na sheria za nchi kama sehemu moja ya kupanua na kuongeza kina cha watu kujitawala, kujiamulia mambo yao wenyewe na demokrasia kiujumla.
Chama tawala kina unafiki mkubwa ambao ni muhimu kuutambua na kuubainisha kwa wadau wa katiba. Kwa kuwa kinatambua nguvu yake inatokana na ujinga, umaskini na magonjwa mbalimbali ya watawaliwa basi kinaelewa fika kuwa kupiga vita mambo hayo ni lazima wanajamii washirikiane ili kufanikiwa. Lakini, ushirikiano wa wananchi kijamii na kiuchumi kutawapa pia wanajamii nguvu na sauti sawa au zaidi ya wanasiasa. Kwa mantiki hii chama cha siasa kinachokubali makundi ya jamii au watu kuwa huru zaidi kiuchumi na kisisasa katika ngazi ya mtaa, kata, wilaya na mkoa huhofia pia kujimaliza kisiasa. Kwa sababu hii, maamuzi yote yanayohusiana na kuyapa makundi ya kijamii nguvu na uwezo zaidi hufanywa polepole mno. Jambo la siku moja huchukua mwezi; la mwezi, mwaka; la mwaka muongo; la muongo karne kama sio zaidi!

Hata hivyo, ili nchi na watu wake wapate maendeleo hakuna njia ya mkato. Njia ni moja tu. Nayo ni ushirikishwaji wananchi na umilikaji wananchi uchumi wa nchi katika uundwaji wa katiba na sheria za nchi zinazoendana na wakati tuliomo; ushirikishwaji watu katika maamuzi, mipango, uongozi, utekelezwaji na udhibiti wa masuala yote ya maendeleo na ustawi wa jamii husika ikiwemo kuwa na mikoa huru kiuchumi inayokuwa chini ya viongozi waliochaguliwa na wananchi au wakazi wa mkoa husika.

Kwa kifupi kuna mambo kadhaa yanayoonesha wazi kwamba ili serikali yoyote ifanikiwe ni lazima wananchi wake washiriki na wawe na sauti katika uongozi wa nchi:
. Kukubalika, heshima na uwezo wa serikali kuu huanza kwenye mitaa na jamii mikoani;
. Maendeleo ya kweli ya mkoa yanatokana na kile wananchi wake wanachozalisha na kumiliki na sio vitu vya wageni;
. Serikali zenye nguvu na uwezo za mikoa na mitaa hufanya kazi ya kulinda hazina ya mkoa na mali asili za eneo husika kwa faida ya wakazi wake na nchi nzima;
. Uongozi wa kitaifa hutekeleza miradi ya mikoa aghalabu nusu nusu na bila udhibiti wa kutosha kutokana na kukurupuka na kwenda kuzima moto unaowaka mkoa mwingine, hivyo kuhamisha fedha kwa ajili ya mkoa mmoja kwenda kuufaa mkoa mwingine isivyo haki;
. Serikali huru za mikoa ni shule au chuo pekee kitakachowafundisha viongozi wa baadaye wa kitaifa kwa vitendo huko huko waliko mikoani.

Migogoro ya kisiasa inayotokea Afrika na hususan Tanzania kwa kiasi kikubwa ni kati ya wale wamanaoamini:

* Wanasiasa wanaoamini kwamba Watanzania ni waoga na wasiokubali tofauti kati yao na migogoro na wale wanaoamini Watanzana ni mashujaa na kuwa tofatui na migogoro ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni ni sehemu ya maisha ya kawaida ya nchi na wananchi na lazima ikubalike na itumiwe kwa faida ya kunusuru nchi na watu wake;
* wanasiasa kazi yao ni kutawala na wananchi ni kutawaliwa tu dhidi ya wale wanaoamini wananchi wanastahili kujitawala wenyewe;
* Wanasiasa wanaoamini viongozi wetu wanastahili kuishi kifahari na wale wanaoamini ni lazima wanasiasa wajishushe kwanza na kuwanyanyua watu wao kabla ya wao wenyewe kuwa na maisha mazuri na bora;
* Wanasiasa wanaodhani kuwa kazi ya vyombo vya habari vya umma na vile vya chama tawala ni kufumua na kuharibu ukweli na kisha kufuma na kusambaza urongo na wale wanaoamini hakuna mwenye haki ya kutengeneza na kuuzia wananchi uongo Afrika;
* wanasiasa wanastahili maisha mazuri na bora kuliko raia wengine na wale wanaoamini wananchi wanastahili maisha bora na mazuri kuliko ya wanasiasa;
* wanasiasa wetu wanastahili kuwanyenyekea na kuwafuata wale wanasiasa matajiri kwa kila jambo wanalolisema au kutushauri hata likiwa halina maslahi kwa watu wetu na wale wanaoamini wakati umefika kwa wanasiasa wetu kusimama kwa miguu yao wenyewe;
* wanasiasa wanastahili kuwatumia polisi na pengine jeshi ili kuwasaga wananchi waende kule wao wanakotaka waende dhidi ya wale wanaoamini polisi na jeshi wanastahili kudhibiti wanasiasa kwenda kule katiba na wananchi wanakotaka nchi iende;
* wanasiasa wanahitaji kubaki madarakani milele ili walete maendeleo na wale wanaoshani wanastahili kubaki tu madarakani kama wanaweza kuongeza thamani na ubora wa miasha ya mwananchi;
* wanasiasa wanaoamini wananchi wakielimishwa na wakiondokana na ujinga na umasikini itakuwa vigumu wao kutawala dhidi ya wale wanaoamini itakuwa rahisi zaidi kwao kutawala;
* Wanasiasa wanaoamini wananchi ni wajinga na wao wanasiasa ni wajanja na wale wanaodhani hakuna kitu kama hicho na jambo hilo linategemea watu binafsi na mitazamo na makusudio yao;
* wanasiasa wanaoamini ni wanachama wa chama fulani tu wanaostahili kuwa na sauti na kuwa makundi mengine katika jamii hayastahili kuwezeshwa wala kuwa na nguvu iwe ya kisiasa, kijamii au kiuchumi na kadhalika;
* wanasiasa wa chama tawala ndio tu wapewe uongozi hata kama hawawezi kazi na wale wanaodhani wanaostahili kuongoza wananchi lazima wachaguliwe na wananchi wa eneo husika.

Afrika imebadilika, na Afrika ya leo si ya jana. Wale wote wenye fikra hasi pacha za kwanza hawana tena nafasi katika Afrika mpya. Kizungumkuti kinachokuja kitawafagia pembeni hadi kwenye majaa kama ilivyofanyika huko Maghreb na kuwajaribu wala wenye fikra mbadala chanya pacha hapo juu.

Na njia sahihi ya kuifuata ni kuhakikisha kuwa kuanzia sasa tunakubali na tunahamasisha kupeleka madaraka kwa wananchi sio tu mikoani bali mpaka vijijini na kwenye kila kata na mtaa.

Mikoa Huru ya Ujerumani:
Kwa mfano mikoa ya Ujerumani ni pamoja na Baden-Württemberg, Bavaria (Bayern), Berlin,Brandenburg na Bremen. Kahalika kuna Hamburg, Hesse
(Hessen), Mecklenburg-Vorpommern, Lower Saxony (Niedersachsen), North Rhine-Westphalia (Nordrhein-Westfalen), Rhineland-Palatinate (Rheinland-Pfalz), Saarland, Saxony (Sachsen), Saxony-Anhalt (Sachsen-Anhalt), Schleswig-Holstein na Thuringia (Thüringen).

Mikoa yote hii isipokuwa kwa mkoa mmoja tu ina serikali za pamoja/mseto kati ya vyama viwili au zaidi. KIla mkoa una waziri wake mkuu, baraza lake la mawaziri, wawakilishi wake na taasisi zake na inakuwa huru kwa kiasi kikubwa kwenye masuala yote ya kiuchumi na kijamii. Yale ya ulinzi, usalama, fedha na siasa za nje hushughulikiwa zaidi na serikali ya kitaifa yenye makao yake makuu hivi leo Berlin. Mikoa hii imewezesha kuwa na ushindani wa ndani kwa ndani na hivyo kuipa nguvu Ujerumani katika utandawazi na ushindani wa nje kwa kujikita tu kwenye maeneo inayoamini hakuna anayeweza kuwapita. Wao si watu wa kufanya na kujaribu kila kitu kwa kubahatisha. Hutafuta uhakika kwanza kabla hawajawekeza kwenye jambo fulani.

Jiografia ya nchi na rasilimali

Baadhi ya mambo yanayofanyika nchini hivi leo hayaashirii mshikamano na umoja wa nchi.

Kwa mfano, badala ya kujenga vyuo vikuu vidogo kila mkoa serikali iliyopo madarakani ina mkakati wa kujenga vyuo vikuu vikubwa katika mikoa michache iliyochaguliwa kwa sababu zisizofahamika. Hili linafanyika ikidhihirika kuwa bado hatujawa na rasilimali watu timilifu kusimamia vyuo vikubwa vyenye wanafunzi zaidi ya elfu tano tu. Hali kadhalika, hili linatokea wakati kila mkoa unajenga hisia ya kupendelewa au kutopendelewa katika kupata taasisi kama hizi. Je, huko mbele tunakokwenda hakuna mikoa itakayokuja kugeuka na kudai vyuo vikuu vilivyopo mkoani vyake ni vyake na sio vya kitaifa. HIvi tumejifunza nini toka Yugoslavia na Urussi ya zamani na yaliyotokea huko? Aidha, mkoa kukosa kabisa angalau chuo kikuu kimoja ni dhuluma ya hali ya juu ya kielimu kwa wakazi wa mkoa husika. Kwa maneno mengine kama Tanganyika ilivyoanza na Chuo KIkuu chenye chini ya wanafunzi mia moja basi ni haki ya kila mkoa kuanzisha chuo kikuu chake hata ikiwa ni kuanza na wanafunzi ishirini tu. Kitaongozwa vyema. Kitakuwa. Kitaendelea na mkoa utajivuna pia kuwa na chuo kikuu chao.

Hili limerahisishwa tayari na Chuo Kikuu huria cha Tanzania (CKT) kinachotakiwa ni kukisaidia chuo hicho sasa kugeuza matawi yake mikoani kuwa k.m. Chuo KIkuu Huria cha Arusha au Manyara au Mbeya au Ruvuma au Pwani na kadhalika.

Sunday, February 27, 2011

Mikoa Huru na Udikteta Chipukizi

UDIKTETA au ukiritimba au mtu kuhodhi mamlaka yote peke yake, iwe kisiasa au kiuchumi au kijamii huashiria kuwa huyo ni mtu au mtu mwenye kikundi cha watu wasiajiamini na wasiokuwa na uhakika na kile wanachokifanya. Aghalabu watu wa namna hii huwa hawajui wanakotoka wala wanakokwenda. Ni mwanzo wa kuficha maovu mengi kwa kuonesha mazuri machache ambayo pengine hayana faida wala manufaa kwa a ya kujichimbia kaburi lake yenyewe. Huanza kwa kutoamini wengine lakini huishia kwa kutojiamini wenyewe na kutoaminiana wenyewe kwa wenyewe na kuishia kujichanganya na kujimaliza wenyewe.

Udikteta huweza kuundwa na mtu mmoja au kikundi cha watu. Udikteta uliopo Tanzania hivi leo ni ule wa kichama. Udikteta huu unajidhirisha kwa chama hicho kutaka kuwa na watu na sauti katika kila jambo hata yale yasiyokihusu- kwa mfano, dini, utamaduni, mila na desturi, mawasiliano, maendeleo ya watu na jamii zao, ushirika, uzalishaji mali na majumuiko mengine ya kijamii kwa hofu hii au ile.
Kwa kuwa wanasiasa waliopo wanaamini kwamba kwa kuwa hawawezi kuitawala nchi bila ya kulazimisha mikoa, wilaya, vijiji na mitaa kuwa chini ya chama tawala basi miundo na mifumo ya kisiasa inayoundwa sio ile ya kufanya maeneo hayo kuwa huru bali maeneo hayo kutawaliwa moja kwa moja au kimzunguko na chama tawala na viongozi wake.
Ni dhahiri basi madaraka mikoani au kuwa na mikoa huru kiuchumi na kijamii sio jambo linaloweza kufanywa na wanasiasa wa chama tawala. Hili ni jambo linalostahili kuwemokwenye katiba na sheria za nchi kama sehemu moja ya kupanua na kuongeza kina cha watu kujitawala, kujiamulia mambo yao wenyewe na demokrasia kiujumla.
Chama tawala kina unafiki mkubwa ambao ni muhimu kuutambua na kuubainisha kwa wadau wa katiba. Kwa kuwa kinatambua nguvu yake inatokana na ujinga, umaskini na magonjwa mbalimbali ya watawaliwa inaelewa fika kuwa kupiga vita mambo hayo ni lazima wanajamii washirikiane ili kufanikiwa. Lakini, ushirikiano wa wananchi kijamii na kiuchumi kutawapa pia wanajamii nguvu na sauti sawa au zaidi ya wanasiasa. Kwa mantiki hii chama cha siasa kinachokubali makundi ya jamii au watu kuwa huru zaidi kiuchumi na kisisasa katika ngazi ya mtaa, kata, wilaya na mkoa huhofia pia kujimaliza kisiasa. Kwa sababu hii, maamuzi yote yanayohusiana na kuyapa makundi ya kijamii nguvu na uwezo zaidi hufanywa polepole mno. Jambo la siku moja huchukua mwezi; la mwezi, mwaka; la mwaka muongo; la muongo karne kama sio zaidi!
Hata hivyo, ili nchi na watu wake kuendelea hakuna njia ya mkato. Njia ni moja tu. Nayo ni ushirikishwaji wananchi katika uundwaji wa katiba na sheria za nchi zinazoendana na wakati tuliomo; ushirikishwaji watu katika maamuzi, mipango, uongozi, utekelezwaji na udhibiti wa masuala yote ya maendeleo na ustawi wa jamii huska ikiwemo kuwa na mikoa huru kiuchumi inayokuwa chini ya viongozi waliochaguliwa na wananchi au wakazi wa mkoa husika.
Kwa kifupi kuna mambo kadhaa yanayoonesha wazi kwamba ili serikali yoyote ifanikiwe ni lazima wananchi wake washiriki na wawe na sauti katika uongozi wa nchi:
. Kukubalika, heshima na uwezo wa serikali kuu huanza kwenye mitaa na jamii mikoani;
. Maendeleo ya kweli ya mkoa yanatokana na kile wananchi wake wanachozalisha na kumiliki na sio vitu vya wageni;
. Serikali zenye nguvu na uwezo za mikoa na mitaa hufanya kazi ya kulinda hazina ya mkoa na mali asili za eneo husika kwa faida ya wakazi wake na nchi nzima;
. Uongozi wa kitaifa hutekeleza miradi ya mikoa aghalabu nusu nusu kutokana na kukurupuka na kwenda kuzima moto unaowaka mkoa mwingine, hivyo kuhamisha fedha kwa ajili ya mkoa mmoja kwenda kuufaa mkoa mwingine isivyo haki;
. Wizi wa kura unaofanyika kirahisi chini ya uchaguzi wa kitaifa utapungua ikiwa kila mkoa unachagua viongozi na serikali yake kwanza wao wenyewe kabla ya uongozi wa kitaifa;
. Serikali huru za mikoa ni shule au chuo pekee kitakachowafundisha viongozi wa baadaye wa kitaifa kwa vitendo huko huko waliko mikoani.

Migogoro ya kisiasa inayotokea Afrika na hususan Tanzania kwa kiasi kikubwa ni kati ya wale wamanaoamini:
. wanasiasa kazi yao ni kutawala na wananchi ni kutawaliwa tu dhidi ya wale wanaoamini wananchi wanastahili kujitawala wenyewe;
. Wanasiasa wanaoamini viongozi wetu wanastahili kuishi kifahari na wale wanaoamini ni lazima wanasiasa wajishushe kwanza na kuwanyanyua watu wao kabla ya wao wenyewe kuwa na maisha mazuri na bora;
. Wanasiasa wanaodhani kuwa kazi ya vyombo vya habari vya umma na vile vya chama tawala ni kufuma na kusambaza urongo na wale wanaoamini hakuna mwenye haki ya kutengeneza na kuuzia wananchi uongo Afrika;
. wanasiasa wanastahili maisha mazuri na bora kuliko raia wengine na wale wanaoamini wananchi wanastahili maisha bora na mazuri kuliko ya wanasiasa;
. wanasiasa wana haki ya kuiba toka hazina za taifa na kuweka fedha toka nchi maskini katika nchi tajiri kwa hifadhi yao ya baadaye na wale wanaoamini huo ni ujinga na kama mwanasiasa ni mwananchi mzalendo hifadhi yake lazima itoke ndani ya jamii yake;
. wanasiasa wetu wanastahili kuwanyenyekea na kuwafuata wale wanasiasa matajiri kwa kila jambo wanalolisema au kutushauri hata likiwa halina maslahi kwa watu wetu;
. wanasiasa wanastahili kuwatumia polisi na pengine jeshi ili kuwasaga wananchi waende kule wao wanakotaka waende dhidi ya wale wanaoamini polisi na jeshi wanastahili kudhibiti wanasiasa kwenda kle wananchi wanakotaka nchi iende;
. wanasiasa wanahitaji kubaki madarakani milele ili walete maendeleo na wale wanaoshani wanahitaji muhula mmoja tu kufanya kazi hiyo;
. wanasiasa wa chama tawala ndio tu wapewe uongozi hata kama hawawezi kazi na wale wanaodhani wanaostahili kuongoza wananchi lazima wachaguliwe na wananchi wa eneo husika;
. wanasiasa wanaoamini wananchi wakielimishwa na wakiondokana na umasikini itakuwa vigumu wao kutawala dhidi ya wale wanaoamini itakuwa rahisi zaidi kwao kutawala;
. wanasiasa wanaoamini kuwa chama cha kisiasa lazima kiwaibie wananchi ili kiendelee kutawala na wanaoamini wananchi wenyewe wanaweza kukika chama uwezo wa kujiendesha;
. wanasiasa wanaoamini ni wanachama wa chama fulani tu wanaostahili kuwa na sauti na kuwa makundi mengine katika jamii hayastahili kuwezeshwa wala kuwa na nguvu iwe ya kisiasa, kijamii au kiuchumi na kadhalika.

Afrika imebadilika, na Afrika ya leo si ya jana. Wale wote wenye fikra pacha za kwanza hawana tena nafasi katika Afrika mpya. Kizungumkuti kinachokuja kitawagia kama ilivyofanyika huko Maghreb pembeni na kuwajaribu wala wenye fikra mbadala pacha hapo juu.

Na njia sahihi ya kufuata kuanzia sasa ni kuhakikisha kuwa tunapelekea madaraka kwa wananchi sio tu mikoani bali mpaka vijijini.

Mikoa Huru ya Ujerumani:
Kwa mfano mikoa ya Ujerumani ni pamoja na Baden-Württemberg, Bavaria (Bayern), Berlin,Brandenburg na Bremen. Kahalika kuna Hamburg, Hesse
(Hessen), Mecklenburg-Vorpommern, Lower Saxony (Niedersachsen), North Rhine-Westphalia (Nordrhein-Westfalen), Rhineland-Palatinate (Rheinland-Pfalz), Saarland, Saxony (Sachsen), Saxony-Anhalt (Sachsen-Anhalt), Schleswig-Holstein na Thuringia (Thüringen).

Mikoa yote hii isipokuwa kwa mkoa mmoja tu ina serikali za pamoja/mseto kati ya vyama viwili au zaidi. KIla mkoa una waziri wake mkuu, baraza lake la mawaziri, wawakilishi wake na taasisi zake na inakuwa huru kwa kiasi kikubwa kwenye masuala yote ya kiuchumi na kijamii. Yale ya ulinzi, usalama, fedha na siasa za nje hushughulikiwa zaidi na serikali ya kitaifa yenye makao yake makuu hivi leo Berlin. Mikoa hii imewezesha kuwa na ushindani wa ndani kwa ndani na hivyo kuipa nguvu Ujerumani katika utandawazi na ushindani wa nje kwa kujikita tu kwenye maeneo inayoamini hakuna anayeweza kuwapita. Wao si watu wa kufanya na kujaribu kila kitu kwa kubahatisha. Hutafuta uhakika kwanza kabla hawajawekeza kwenye jambo fulani.

Wednesday, February 9, 2011

Utalii, Tanroads na Kujipanga Kimkakati

MAJUMA mawili yaliyopita, siku ya Jumanne, kulikuwa na habari za Kenya kujenga bandari na kiwanja cha ndege mpakani mwa Tanzania. Hili linatokea wakati ambapo mwaka mmoja haujapita toka makala haya kuhoji kuwepo kwa 'bodaposti' katika mipaka yetu ambazo zimefanana sana na vichaka bodaposti hizo zilizomo.

Makala haya yakashauri kwamba wakati umefika sasa kubadilisha bodaposti hizo zifanane na viwanja vya ndege vya kimataifa ili kuwapendezesha na kuwavutia zaidi watalii na wawekezaji kuja kusaidia kukuza na kuendeleza uchumi wetu. Kitu ambacho ni haki yao. Wakati Kenya walisoma, kuitafakari na kuifanyia kazi habari hiyo wenzetu bado wapo usingizini na hakuna kinachoendelea. Bado somo la utandawazi na ushindani usio na mipaka halijaeleweka hata kidogo kwa upande wao.

Kenya inatambua fika kwamba vivutio vikubwa vya utalii hapa Afrika Mashariki viko Tanzania. Walichokifanya ni kutumia akili yao kwani wanajua Watanzania hawatumii zao ila kwa yale yasiyochangia maendeleo yao bali kuyavuruga na kuharibu walichonacho. Nchi ya maneno mengi sana, lakini ya vitendo vifupi na vichache mno, ndivyo tunavyoitwa eti! Nani wa kubisha ?

Kiutalii tunakwenda wapi ?

Hivi kweli tunataka utalii uchangie kupunguza umaskini nchini ? Nina mashaka. Maana tungelikuwa na busara hiyo yale yaliyofanyika Arusha ambayo ni kitovu cha utalii yasingefanyika. Lakini hilo ni dogo tu. Tuje kwenye picha kubwa. Hivi kujitangaza Ulaya, Marekani na kwenye CNN na wengineo kama hako kutatusaidia kweli bila kujipanga hapa nyumbani ? Muhali sana.

Takwimu zinaonesha sekta ya utalii inakuwa haraka kuliko sekta za mazoea za siku za nyuma. Lakini kukua kwa utalii hapa nchini kutategemea sana jinsi tunavyoondokana na picha ya sisi kuwa nchi masikini. Kwa kadri tutakavyoonekana ni masikini (wa kujitakia) tutawaogopesha watu kuja kutalii nchi hii. Na kwa ujumla watu wasiotaka kubadilika na wanaotaka kuvuna pale wasipopanda kitu chochote. Ni lazima serikali ishiriki kikamilifu katika uendelezaji wa sekta hii ili iweze kufanya maajabu katika muda mfupi iwezekanavyo. Na njia mojawapo kama nilivyosema ni ile ya kuwa na mikakati sahihi ya kupunguza kama sio kuundoa kabisa umaskini wa kutupwa.

Tanroads na Wizara husika zijipange upya

Kama kweli tunataka utalii utusaie kupunguza umaskini ni lazima tujipange upya. Ninachokiona sasa ni kuwa wahusika wakuu kila mmoja anakwenda njia yake na analifanya lile analojua yeye. Hili nadhani ni kosa. Ninashauri wale wanaoishi kando ya barabara zetu, Tanroads, SUMATRA, Kituo cha Uwekezaji Tanznia, NSSF, PPF, Wizara ya Utalii, TANAPA, Wenye vyombo vya usafiri, Wasafirishaji Watalii, Wenye mahoteli wafanye kazi pamoja ili barabara zetu zisiwe kama mstari tu unaopita juu ya nchi baliziwe na vivutio vya aina mbalimbali vitakavyogeuza njia husika yenyewe kuwa ni kivutio cha utalii pia.

Tuchukulie mfano wa barabara mbili kuu Tanzania, yaani, ile ya Dar es Salaam-Arusha/Namanga na ile ya Dar es Salaam-Mbeya/Tunduma. Barabara hizi zimejengwa kizamani. Hazina mvuto kwa watalii ila vivutio vya asili na vile vichache watu binafsi walivyoviweka njiani. Lakini hebu tujiulize walichokifanya waliojenga hoteli pale Kitonga na pale Highway Korogwe kimeongeza ubora wa huduma za usaifi njia hizo kwa kiasi gani ? Na, je, mifano hii inaweza kuigwa kwenye mambo mengine ? Je, tunaweza kuwa na sehemu zenye huduma zote muhimu kama vile misikiti au mahala pa kusalia, zahanati, vituo vya mafuta, vyombo vya ulinzi na usalama, mahoteli, viwanja vya michezo mbalimbali,mabwawa ya kuogelea, vyoo safi, bafu, gesti, intaneti, simu, maduka, masoko na kadhalika kwa kila kilomita 70 hivi? Mathalani njia ya Dar-Arusha ukawa na vituo kama hivyo 5 na ile ya Dar-Mbeya kama 10 hivi ? Ninaamini kuwepo barabara kunakuwa na faida endapo watu wanafaidika na barabara hiyo na biashara na miji mipya inazuka. Kazi ya kwenda kuchimba dawa ikiisha hivi kuna mgeni atakayesita kusafiri na mabasi ya TABOA ?

Tujiulize, ni kwa namna gani tutaacha kujenga barabara zisizokuwa na kivutio chochote njia nzima? Maana zikibaki kama zilivyo zinakuwa hazijaongeza thamani wala maslahi yoyote ya maana kwa Mtanzania wa kawaida. Na utunzaje wake pia hapo baadaye unakuwa wa mashaka. Njia bora ni kuwa na ushirikiano na washikadau wote katika kuzifanya barabara zetu na maeneo zinakopita kuwa ni aina fulani ya kivutio cha utalii. Kiasi kwamba mtu anaposafiri kuelekea Arusha au Mbeya asitake kufika huko haraka na ikiwezekana alale siku mbili au tatu njiani kufaidi vivutio mbalimbali anavyokutana navyo njiani. Kwa namna hii pia utalii sasa utashuka hadi chini na kuwanufaisha masikini ili mradi tu twende nao sambamba katika kuhakiki viwango vya ubora vinavyokubalika njia nzima.
Utalii ni kama msichana. Jinsi anavyokuwa mzuri, msafi, mwenye kujua mapishi ya kila aina, mcheshi na mwenye kuvutia kwa kila hali ndivyo wanaume wengi wanavyojigonga gonga kwake kila kukichwa!

Humo mote barabara hizo kuu zinamopita inawezekana kuwa na programu kamambe ya kukuza utalii wa aina mbalimbali ukiwemo ule wa makumbusho, vyakula na vinywaji, miti na mali asili zingine. Aidha, utalii wa kielimu, mafunzo, mikutano na kiutafiti pia unawezekana na ile ya anasa au starehe, michezo na sanaa. Vilevile utalii wa usafi na mazingira bora, mazoezi, tiba na afya na kadhalika.

Kama hili litaendana na kuondokana na bodaposti za kale na badala yake kuwa na vituo vya mpakani sawa na viwanja vya ndege kwa ushirikiano kati ya wananchi, serikali na wawekezaji wa nje na ndani kilichofanywa na Kenya kinaweza kikawa ni hasara badala ya faida. Isipokuwa hakuna muda hata kidogo wa kusubiri. Kama walivyosema wahenga: " Chelewa, chelewa utamkuta mtoto si wako!"

Tanroads isifikirie kiuhandisi au kifundi tu. Ianze kujenga tabia ya kufikiria mambo kibiashara na kiuchumi. Upo uwezekano mkubwa sana wa barabara zetu kusaidia kupunguza umaskini endapo miradi kama iliyooneshwa hapo juu itatekelezwa inavyostahili na sio kiubabaishaji.

Sambamba na hili ni lile la kuwa na barabara moja kuu inayotambaa na bahari ya Hindi katika pwani ya Tanzania kiasi ambacho kwamba tunaweza pia kuwa na Utalii wa pwani ya Tanzania kwa meli, ndege na magari. Na katika yote haya nafuu ya kimaisha na kiuchumi ikapatikana kwa wakazi wa maeneo husika katika muda mfupi tu ujao. Mikoa yetu ya pwani kwa kiasi fulani ni masikini na iko nyuma kimaendeleo kwa sababu bahari, vilivyomo na fukwe zake ambazo ndio rasilimali zao kuu hazijatumika ipasavyo kuvutia watalii katika maeneo hayo.

Katika dunia inayobadilika kila siku ni kosa kubwa kufanya jambo bila kuhusisha mambo mengine yanayoendana na jambo hili. Huu ni mtazamo wa kuyafanya mengi kwa faida kubwa chini ya mwamvuli mmoja, kwa maana kwamba, mambo mengi kwa pamoja yanaweza kufanyika kwa faida kubwa zaidi na kwa manufaa ya wengi zaidi kwa wakati uleule.

Ipo kila sababu kama kweli tunataka kuitumikia nchi hii na watu wake kuifanya Tanroads, Wizara ya Mali Asili, Hazina, TASAF, Benki Kuu, mabenki mbalimbali, makampuni ya mafuta na simu za mkononi kuanza kufikiria kuwapa Watanzania nyavu za kuvua samaki wao wenyewe badala ya kuwadanganya na kipande cha samaki au nguru kila siku.

Sunday, February 6, 2011

Tatizo Si Vyama Bali Vijana Kukosa Ajira na Tumaini

Tatizo Si Vyama Bali Vijana Kukosa Ajira na Tumaini

UPO msiba mkubwa Tanzania ambao sio mwingine ila ni ule wa viongozi na wananchi kujenga tabia ya kutangaza, kuamua au kutetea jambo fulani baada ya kumsikiliza mtu mmoja au chombo kimoja tu. Huu ni msiba mkubwa ambao unaweza kutufikisha kwenye gharika ya karne kitaifa katika muda sio mrefu kutoka sasa.

Aidha, pamoja na msiba huo ni ajali za kila siku ambako viongozi wetu hufikia kwenye majibu mepesi na ya kirahisi kwa masuala tata na magumu ya kitaifa na kijamii!

Mifano iko mingi. Tanzania inashinda kombe la chalenji kwa fluki basi nchi bila hata kukuza vipaji vyovyote vya maana wala maandalizi inaonekana tayari imepanda juu kisoka (hebu cheki taarifa ya FIFA ya hivi karibuni-mambo ni kinyume chake). TANESCO wanaomba kuongeza bei na wanaruhusiwa mara moja eti gharama zimepanda. Hakuna maelezo ya
wataalamu kwamba badala ya kupandisha bei TANESCO ingeweza ikapunguza gharama moja, mbili, tatu na isihitajike kupandisha bei umeme. Hakuna anayehangaisha akili ili kuangalia wizi na ubadhirifu TANESCO upo kiasi gani, jinsi gani watu wanajiandikia 'overtime' ya masaa 10 kwa kazi ya saa moja na kadhalika.

Tuliambiwa mgawo wa umeme sasa ni historia. [ Wengine leo wanadai wanahabari walinukuu kauli hiyo vibaya. Eti ni mgawo wa Kihistoriaa na sio mgawo utakuwa historia. ]
Inaonekana bado ni hadithi pevu na mpya kabisa. Kiasi kwamba wakati mwingine kuna watu wanaojiuliza kama viongozi wetu ni watu wazima au watoto wadogo? Inashangaza sana.

Kati ya muda ambao kiongozi anaambiwa kuwepo tatizo au fursa au changamoto fulani hadi anatoa kauli juu ya tatizo hilo kuna mambo kadhaa yanayotakiwa kufanyika. Kwanza, apate habari tofauti kutoka vyanzo mbalimbali. Asiwaamini tu maofisa na washauri wake. Apate watu wa kumfanyia kazi ya ziada pembeni ya wale wanaomzunguka. Atafakari ripoti zote
kwa kina. Akutane na wataalamu wa masuala husika na azungumze nao bila kutumia ukubwa wake kupata msimamo wao wa kweli. Kisha aangalie sasa kutokana na maelezo aliyo nayo anafaa kutangaza au kulizungmza jambo hadharani au la. Na kama ni kulitangaza litangazwe likiwa na mashiko yapi ya kiidhibati, kisheria na kiakili, kibusara na kihekima.

Kukurupuka tu baada ya kushauriwa na mtu au kikundi au taasisi moja mtu akajibu maswali mazito ya kitaifa au kimataifa hakika ni msiba usioelezeka nchini hapa. Na matokeo yake mara nyingi inakuwa ni mtu au nchi kujiiaibisha bila sababu ya maana.

Nikimsikiliza mwanasiasa mmoja machachari Tanzania nilibaki kinywa wazi alivyokuwa akielezea kiini cha tatizo la maandamano na vurugu huko Tunisia na Misri. Sina haja ya kurudia alichokisema, lakini upeo na uwezo wake kama kiongozi ulikuwa rahisi sana kuonekana kwa yeyote mwenye utambuzi na tafakuri kama mtu wa kawaida tu na wala sio lazima
awe mwalimu wa menejimenti na oganaizesheni na sayansi ya maamuzi. Hizi ndizo baadhi ya ajali za nchi yetu ambazo zinatokana na kutotambua umuhimu wa kutafuta katika rasilimali watu zetu kile kilicho bora zaidi kwa kila jambo na eneo.

Kinachotokea Afrika Kaskazini si majibu kwa ukame wa demokrasia na usawa katika ugawanyaji rasilimali za nchi ingawa hizi ni baadhi ya sababu.

Ukikumbuka historia ya ulimwengu kunako miaka ya 1960 na kizazi cha 'baby boomers' na 'mahippies' moja kwa moja unaona uhusiano kati ya matukio ya miaka hiyo na kile kitakachotokea katika muongo huu hapa Afrika.

Hali ya hewa na mazingira katika miaka ya 60 na 70 yamechangia Waafrika kuwa na watoto wengi ambao leo ni vijana. Baadhi ya vijana hawa wamezaliwa, wamesoma chekechea, shule ya msingi na sekondari, chuo kikuu na kuishia joblesi mitaani chini ya rais mmoja au wawili au chini ya chama kimoja tu cha kisiasa. Na hao waliokuwa madarakani hawana cha maana walichokifanya kama wenzetu wa Asia na Marekani Kusini kuinua nchi zao kiuchumi na kijamii.

Vijana hao ambao sasa wana miaka 20-40 wameona wazazi wao wakiwa na maisha bora kuliko waliyokuwa nayo wao leo; wameona jinsi viongozi wanavyozidi kujitajirisha; wameona viongozi wanavyowapa wanawake na watoto wao utajiri na nafasi katika utawala; na wameona jinsi nchi zao zinavyoporwa na kuibwa na viongozi wao wenyewe. Na wamefikia mahala wamechafukwa na roho, moyo na akili kiasi kwamba wako tayari wakipepewa na upepe mdogo tu kuwasha moto mkubwa unaoweza kuangamiza jamiii nzima.
Amani na umoja ambao kwa kawaida unakuwa ni wimbo wa vyama vikongwe vilivyotawala Waafrika sasa unakuwa ni wimbo unaowakinaisha na kutokuwaogopesha kabisa vijana.
Vijana wanajua fika amani wala umoja ni muhimu. Lakini kukosa ajira kwao ni kukosa umoja na kukosa riziki kwao ni kukosa amani. Na kukosa matumaini katika maisha ni kukosa mshikamano kabisa na jamii mtu aliyemo.

Hawa ni watu ambao wamekulia chini ya chama kimoja au rais mmoja toka walipozaliwa, kusoma chekechea, kusoma shule ya msingi, sekondari na hata chuo kikuu. Na sasa ni joblesi na watu wasio na matumaini chini ya chama au rais huyohuyo ! Na televisheni, redio, intaneti na simu za mkononi zinawafungua macho kila siku kuwa mtu au chama kimoja kikitawala kwa muda mrefu kinazeeka, kinachoka na kinaridhika na hali ilivyo hata kama kwa kufanya hivyo kuna mateso, dhiki na majonzi makubwa mioyoni mwa walio wengi.

Katika lugha ya kiutafiti tatizo hili la vijana limeelezwa na watu kadhaa kama David Bloom na wenzake kuwa ni tukio la kinchi linaloitwa 'demographic dividend' au mgawo wa ziada wa kimaendeleo unaoletwa na kuwa na watu wengi wenye umri wa kufanya kazi kuliko wasiofanya kazi. Ikiwa viongozi wanaliona hili na kulifanyia kazi ili nguvu na akili hizo zitumike
kuijenga na pengine kuitajirisha nchi basi nchi itakuwa na amani na maendeleo.
Wasipoliona jambo hili na kadri idadi kubwa ya vijana wanavyokuwa hawana kazi na hawachangii lolote la maana katika maendeleo yao binafsi, ya familia zao na ya nchi basi kulipuka na kusambaratika kwa nchi husika ni kitu kisichoepukika. Kwa maneno mengine, 'demographic dividend' hustahili kuwa kitu cha manufaa kwa nchi na watu wake, lakini
chini ya uongozi mbovu, unaoifilisi serikali yake yenyewe, uongozi unaofikiria kuneemeka wenyewe kwanza na sio wananchi na utawala usiojua unakwenda wapi na unafanya nini jambo hili hugeuka kuwa tani za fataki hatari kwa jamii na nchi nzima.

Baadhi ya dhiki na matatizo yanayowakera vijana wa Kiafrika ni pamoja na kushindwa kujikimu wenyewe na kutegemewa wazazi na watu wengine; kuiona nchi yao inakuwa shamba la bibi la wageni; kuona ndani ya serikali kuna wizi na ufisadi wa kutisha; kuona hakuna dalili zozote za uongezwaji au uzalishaji wa ajira mpya nchini; kubebeshwa zigo la gharama za elimu na afya na kudhulumiwa hata kile wanachotakiwa kupewa au kukopeshwa.

Matatizo mengine ni pamoja na dini na madhehebu mbalimbali kukosa dhamira ya kweli kufuta umaskini na kuwasaidia vijana mitaji, mafunzo na uwezeshwaji wa aina mbalimbali ili waweze kujiajiri; miradi mingi ya serikali ya kijamii kuwa ni ya kuwapa watu samaki badala ya kuwapa nyavu; nchi kushindwa kutumia fursa za kiuchumi zilzoletwa na intaneti na teknolojia mpya; viongozi na matajiri kuwapendelea watoto wao kwanza kwa kila kitu na suala la maendeleo na nafuu vijijini kwa vijana na wazee kuchimbiwa hali hai katika kaburi la sahau serikalini na katika vyama vya kisiasa.

Dini na madhehebu yaliyoanzisha shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu vilitarajiwa vitatoa elimu kwa bei nafuu zaidi na hasa ukizingatia kwamba dini hizo zinapewa sio tu ruzuku na serikali bali pia na nchi za nje. Kinyume chake, shule za kidini leo zinatisha kwa gharama kubwa, walimu duni na wachache, wababaishaji katika menejimenti ya shule, walaji wazuri
tu lakini wanaowalisha wanafunzi chakula sawa au pengine chakula duni zaidi ya kile cha wafungwa magerezani. Shule hizo za kidini zimegeuzwa ni vyuo vya kuvumilia shida na taabu za kila aina.

Mashirika binafsi na yale ya umma yanajali zaidi kutoa ajira kwa watoto wa wakubwa na matajiri lakini wasiokuwa na majina hawafikirii wala kupewa msaada wa kujiendeleza.

Wanaoshika nafasi za uongozi serikalini wanajli zaidi kuwanufaisha watoto, ndugu na jamaa zao na sio kila kijana wa Kitanzania.

Ili kukabiliana na hali hii ni vyema wananchi wakashinikiza viongozi na vyama vya kisiasa na serikali zao kuhakikisha vitendo sasa viwe vinatangulia kauli. Serikali na wanasiasa wafanye kazi kwanza kuleta nafuu kwa watu ndio maneno yafuate. Ieleweke kwamba hakuna kitu kinachomkatisha tamaa mwanadamu kama vile kupewa ahadi hewa au isiyotekelezwa. Hesabu za haraka haraka zinaonesha kuna ahadi zaidi ya 100 zilizotolewa na wagombea nafasi ya Urais nchini. Kama hivyo ndivyo ni hatari kuachia mambo kwenda kama kawaida bila kuwa na taarifa zinazotoka kila mwezi kuonesha ahadi hizo zinaendeleaje kutekelezwa. Na ahadi zenye uzito hapa ni zile ambazo kwa namna moja au nyingine zinakuwa na manufaa kwa vijana.

Tatizo la ahadi zetu nyingi ni kuwa zinachukua miaka mingi hadi kutimizwa. Tunapaswa kujiangalia na kupanga ahadi kutokana na muda unaohitajika. Ahadi ya kukipa kijiji maji ya kisima isichukue mwaka bali ichukue mwezi mmoja au miwili tu. Shule ikikosa madawati au viti lisiwe jambo la mwezi bali la wiki moja tu. Na pale ambapo jambo kweli linataka miezi kadhaa au miaka liwe ni jambo ambalo kila mtu anakubali kwamba haiwezekani vinginevyo.

Wanasiasa wetu kihistoria hawaheshimu muda. Lakini lazima tubadilike tuwe tunaheshimu na kuuchukulia muda kuwa ni rasilimali adimu kuliko zote duniani. Ahadi lazima zimfae yule anayeahidiwa. Tukishakufa ahadi wala maneno mazuri hayatusaidii kitu. Tutekeleze mambo mapema na kwa wakati ili watu wafaidi tunayoahidi wakiwa hai na sio wakishakuwa wafu. Na hili ndilo linalowatisha vijana. Wanaogopa kwamba hakuna ahadi itakayotimizwa wakati wakiwa hai. Au zikitimizwa watakuwa wazee na hawatafaidika tena na kitu chochote kutokana na uzee na kukosa nguvu na uwezo mwingineo.

Ni muhimu pia kwa vijana wa Tanzania kuanzia sasa kuwa na jumuiya ya kitaifa badala ya jumuiya za kichama ili kuepusha tunayona yakitokea Misri na kwingineko baadaye. Kwanza, kuwagawa vijana katika makundi mbalimbali ni kuwazuia kuwa na umoja wa kitaifa na nguvu na sauti zaidi katika maamuzi ya nchi. Lakini muhimu zaidi ni kuwa vijana wakiwa chini ya Muungano wa Vijana wa Tanzania na sio wa chama hiki au kile watajenga Uzalendo na Utanzania wao kuwa madhubuti zaidi kuliko vinginevyo.
Taasisi kama JKT iliundwa makusudi kuwaleta pamoja vijana wa Kitanzania na kuwafanya wote (masikini kwa tajiri,dini mbalimbali, kabila mbalimbali) kujiona wao ni Watanzania kwanza juu ya kitu kingine. Tukiiachia fursa hii kupotea tutakuja ijutia baadaye.

Nimalizie kwa kusema kwamba, Tanzania haijafikia zilipofikia nchi za Maghreb lakini hatuko mbali sana kama tusipoamka na kubadili muundo wa serikali, mifumo ya uendeshaji nchi, matumizi ya rasilimali za nchi na kuacha kuwatanguliza matajiri, wanasiasa na wageni mbele badala ya kumtanguliza Mtanzania mzawa kwanza.

Ni lazima pia tufanye mambo yetu tofauti na watu wengine. Utofauti huu peke yake ndiyo unaoweza kutufanya tuwe tofauti na pengine kufanikiwa kwa haraka zaidi kuliko Waafrika wengine. Tuna mbegu, ardhi na maji tosha kupanda na kuvuna nchi yenye amani, mshikamano na maendeleo kwa wote. Watakaosababisha mambo kuwa kinyume cha hivyo wamo miongoni mwetu na ni wale wasiojua nchi hii na watu wake wanatakiwa waelekee wapi!

Kila mtu anaafiki Tanzania ina viungo vyote nchi inayohitaji kuandaa pilau safi ya ustawi jamii; uchumi imara; lugha ya Kiswahili inayoweza kumfundisha Mtanzania kila kitu chini ya mbingu; ustaarabu; miji safi na yenye mvuto kwa walio ndani na nje; kilimo kinachotutosheleza na ziada kupatikana; viwanda maridhia kukidhi mahitaji yetu ya ndani na ya nje; utalii wenye vivutio aali na vingine vya kutengnezwa an watu; taasisi za elimu zinazovutia walimu na wanafunzi toka nje, hospitali zinazovutia madaktari na wagonjwa toka nje, migodi ya madini na mali asili zinazoweza kupunguza nusu ya umaskini wetu na masoko na biashara zinazoweza kutufanya wafanyabiashara bora Afrika na kwingineko -ila kinachokosekana ni wapishi wanaoweza kuikubali kazi yao ya upishi wakakaa jikoni kwa muda unaohitajika na sio kama viongozi wetu ambao wanausahau upishi wao na kukaa mezani chakula hicho kipikwe sijui na nani?

Tuesday, December 28, 2010

Ngazi za Chini za Uongozi Tanzania Lazima Ziwe na Watu Bora...


KUNA tabia iliyojengeka kwa muda mrefu sasa miongoni mwa Watanzania, ikidhihirishwa na baadhi yao kujiona bora zaidi na hawastahili kuwa viongozi wa chini. Wengi wetu hudhani kwamba nafasi au vyeo vya chini katika uongozi sio za stahili wala kiwango chao. Hili ni pamoja na ule ukweli kwamba maendeleo huanzia katika ngazi za chini na sio juu. Aidha, hakuna nchi inayoweza kuwa na maendeleo endelevu bila ya viongozi wazuri na makini katika ngazi za chini.


Kwa sababu wenzetu hao wanajiona wamesoma sana, matajiri sana au tayari wakubwa na wana vyeo vikubwa sana basi wanawaachia watu wasiosoma, masikini na wanyonge nafasi za uongozi katika ngazi za chini kama vile usimamizi wa nyumba kumi, ukatibu kata, uenyekiti wa mitaa na udiwani. Wao wote wanakimbilia kuwa wabunge, wawakilishi na maraisi japo wanajua fika nafasi hizo ni chache mno na kwamba uongozi si lazima uwe mbunge au waziri au rais wa nchi. Mfano mzuri, tazama bendera za viongozi wa chini zinakopepea huko mitaani. Kwa kiasi kikubwa ni za watu walalahoi mno na ambao umaskini wao hautoi changamoto yoyote ya maana ya watu hao kushughulikia matatizo ya watu wengine.
Kwa upande mwingine chukulia mfano wa matatizo ambayo Zanzibar inayo na kisha kuangalia jinsi huko Zanzibar wagombea wengi ukilinganisha na idadi ya watu wa visiwa hivyo wanaojitokeza kugombea urais na nafasi nyingine za juu.

Wengi wa wagombea hao kama ukiangalia matatizo yanayoizunguka Zanzibar huachi kujiuliza mbona watu hao hao wangelifaa kuwa wakuu wa hiki au kile lakini kwa sababu moja au nyingine wote wanautaka ukubwa wa juu zaidi nchini mwao.

Bnafsi, ninaamini mtu anaweza kuwa waziri, waziri mkuu na hata rais na ili mradi ana nguvu na uwezo wa kubadili maisha ya wananchi wenzake basi akikosa nafasi hizo asisite kukubali kuwa balozi wa nyumba kumi kumi, katibu tarafa au kata, mkuu wa wilaya au mkoa ili wale watakaokuwa chini yao wawe na mengi sana ya kujifunza toka kwa watu kama hao.

Ukizingatia jinsi nchi sasa inavyobahatika kuwa na viongozi vijana basi kila mmoja wao akistaafu na kubakia kula pensheni, nchi inaweza kujikuta ina mzigo usioweza kuubeba katika kuwalea viongozi wastaafu. Pengine ni bora kama utafiti ungelifanyiak hivi sasa kuona inatugharimu nini katika kuwalea viongozi wastaafu waliopo hivi sasa.

Funzo ambalo ningelipenda lijulikane asubuhi na mapema na dhamira kuu ya insha hii ni kwamba bila kuwa na viongozi walioelimika, walioridhikia kimaisha na wanaojua kutofautisha kati ya kutumiwa na viongozi na kuongoza wenyewe nchi hii haitaondokana na umasikini wa kutupwa kwa miaka mingi ijayo.

Kwa maneno mengine, mapinduzi ya kweli ya kiungozi yatakuja tu pale tutakapokuwa na viongozi wa ngazi za chini wanaojua uongozi, uchumi, nadharia tofauti za njia, mbinu, mikakati ya maendeleo na elimu zinazoendana na masuala kama hayo. Viongozi watakaoweza kuzungumza na wageni toka nje bila kusita kwa kuwa hawajiamini na hawana uwezo wa kujieleza, ili waitumie nafasi kama hiyo kuleta maendeleo kupitia uwekezaji na misaada moja kwa moja kwenye maeneo yao.

Hawa watakuwa ni viongozi wanaoweza kuunda baraza la mawaziri la mkoa na ambao wanaweza wakahoji maamuzi yanayofanywa na bunge la taifa na baraza la mawaziri la taifa kwa kuwa wana elimu sawa na walioko juu, ingawa wao zaidi ni katika lugha mama ya taifa, Kiswahili.

Kama nchi hii ingelikuwa inajali lugha yetu mama, yaani, Kiswahili, kufikia wa leo angalau vyuo vikuu vya vyama vya kisiasa tayari vingelikuwa na uwezo na utaratibu wa kutoa shahada za kwanza na za uzamili katika lugha ya kiswahili katika masomo kama uchumi, menejimenti, biashara, uongozi au usimamizi rasilimali watu, bajeti na fedha, mipango na masomo kama hayo.

Kiasi ambacho viongozi wa serikali za mitaa ambao kimsingi wanahitajika hapa hapa nyumbani hawakwamishi kwa sababu ya lugha kupata shahada yao ya kwanza na ya uzamili katika lugha yao ya kazi ya kila siku.

Ni muhimu pia kwa serikali yetu kusaidia na kuviunga mkono vyuo vikuu vya kibinafsi, kijumiya na kidini vinavyotaka kutoa shahada kwa lugha ya Kiswahili ili kusaidia katika kazi hii muhimu nchini.

Isitoshe uongozi wa namna hii ukipatikana katika ngazi ya chini kabisa itakuwa ni rahisi kutathmini viongozi na kuwapa dhamana kubwa zaidi kulingana na mafanikio yao katika ngazi za chini.

Chini ya Uongozi wa kijamaa Watanzania wengi waliokuwa na elimu, vyeo na mali walikataa katakata kugombea nafasi za ujumbe wa nyumba kumi, udiwani na uongozi wa mitaa. Ikawa ni kawaida kwa nafasi hizo kuchukuliwa na watu wasiokuwa na elimu au wenye elimu ndogo sana; wasiowahi kushika cheo chochote na waliokuwa wanaongoza kwa umasikini na hali ngumu ya maisha katika mitaa yao.


Hali hiyo ukienda leo kwenye mikoa mbalimbali na hasa huko vijijini bado ipo na inaendelea. Swali la kujiuliza ni kwamba ikiwa familia, mitaa na vijiji ndio msingi au matofali ya msingi ya taifa leltu hivi kweli tunaweza kujenga taifa lililo imara kisiasa na madhubuti kiuchumi, kijamii, kitekonoojia na kijeshi endapo uongozi wake unashikwa na watu sampuli hii?

Ieleweke kwamba, siwadharau hata kidogo wale walioshika dhamana hii pale ambapo matajiri, wasomi na watu wengine wenye majina walipoidharau na kuikataa. Ila kutokana na mabadiliko ya wakati ambapo sasa Tanzania ni sehemu tu kiuchumi katika ulimwengu mkubwa zaidi naona upo umuhimu wa kujitazama na kujipanga upya ili tuweze kuzikabili changamoto mbalimbali za maendeleo zinazotukabili.

Pengine kuna kosa la kiufundi lililofanyika katika ugawaji dhamana na maslahi yanayoendana na hili. Hivi anayestahili kulipwa mshahara mzuri ni kiongozi wa ngazi ya chini kabisa (ambaye anaweza kuibadili hali ya watu wake toka umaskini au daraja la tatu wakawa la pili au la kwanza) au kiongozi wa ngazi ya juu ambaye nadra kuwa na mawasiliano na wananchi huko waliko? Na kiongozi kama huyo anaweza akaingia na kutoka madarakani bila kubadili hali ya mwananchi yeyote isipokuwa hali yake yeye mwenyewe na jamaa zake ?

Ukweli ni kuwa viongozi wetu wa nyumba kumi, wenyeviti wa mitaa na makatibu kata wote elimu yao , uzoefu wao, uono wao na ufahamu wao wa dunia ya utandawazi bado uko chini kwa upande mmoja. Kwa upande wa pili maslahi na motisha yao ya kuleta mabadiliko ya kimsingi katika jamii zao ni sawa na hamna au ni kidunchu mno. Hii haina tofauti na mameneja, makocha na viongozi wengine wa timu ya michezo kulipwa mara kumi au ishirini ya wachezaji halafu timu ikawa inadorora mwaka nenda, rudi - halafu unatafuta mchawi nje yenu! Kwa maneno mengine, unakuwa mchezo wa Chelsea dhidi ya Arsenal. Mmoja anatumia mabilioni kwa wachezaji, lakini anafungwa na anayetumia vijisenti tuchache tu kujenga kina Daudi wanaomkata kichwa Goliath!

Viongozi au watu wanaoitwa viongozi katika ngazi za chini kwenye nchi hii ni watu wasiolipwa mishahara; hawana elimu ya kutosha kuongoza na kuleta mabadiliko katika jamii; hawana ari, motisha wala moyo wa kufanya kazi; hawana ujuzi na uzoefu katika kazi wanazozifanya na wala hakuna taasisi iliyojipanga au kupangwa kuwafunza na kuwaendeleza.

Viongozi hao wa chini wengi ni masikini kiasi cha kutisha kiasi ambacho sio tu wana vishawishi vingi bali pia wanakuwa sio amana bali deni kwa taifa na hasa pale wageni toka nje ya eneo lao au nje ya nchi wanapokuja na kitita cha fedha na kuwashawishi zaidi. Au wanapotishwa na viongozi wa ngazi ya kitaifa hadi kuwadhulumu na kuwaonea watu wao wenyewe. Ndio maana, habari za wenyeviti au makatibu kuuza ardhi au mali nyingine ya vijiji bila kufuata taratibu na sheria ni kitu cha kawaida katika maisha yetu.

Hata tupate viongozi wa kitaifa ambao wote ni maprofesa, lakini huku chini tuna watu wasiosoma, masikini na wenye ujuzi sawa na hamna katika masula ya uchumi, biashara, uwekezaji, ujasiriamli, menejimenti, usimamizi wa fedha, sheria na kadhalika nchi yetu haiwezi kamwe kuendelea.

Tutajenga kama mataifa mengine yaliyopotea kizazi cha viongozi wanaorithiwa na watoto wao. Ni mwanzo wa kuwa na nchi ambayo itakubali na itaendelea kukubali uongozi mbovu kwa sababu mfumo uliopo hauna chachu wala changamoto inayoiwezesha kupata fikra mbadala na viongozi wenye misimamo mitazamo mipya na inayobadilika na wakati.

Kazi zao nyingi hazina usaidizi wa aina yoyote ile ukiwa ule wa zana, fedha au rasilimali watu. Na kwa hiyo, kwa wakati mwingi ni sehemu ndogo ya yale yaliyostahili kuwa majukumu yao yanatekelezwa kikamilifu.

Wrengi wanajiona wanatumika zaidi kisiasa na baadhi yao wanaamini pengine kile walichostahili kulipwa huliwa na wale walio juu yao. Zaidi ya hilo mara chache sana maamuzi yana sauti katika masuala mbalimbali. Kwa hiyo huiona zaidi ni yoyo kuliko watu wenye sauti katika mambo mengi yanayowazunguka. Nafuu kwao huja wakati wa chaguzi kwani ndipo wanapoweza kupambanisha pande mbalimbali na kuzikamua angalau wapate maziwa ya watoto.

Huu ni wakati mzuri wa kujiuliza, hivi, kama viongozi wa ngazi za chini wangekuwa na elimu, maarifa na maono sawa na wa juu, majimbo yetu ya uchaguzi yangelikuwa kama hivi yalivyo? Je ni mtaji kwa serikali kwa wananchi vijijini kuwa mbumbumbu wa faida za siasa za ushindani? Je, wabunge tunaowapata kwa mfumo huu wa sasa wangelikuwa ndio hao hao katika mazingira ambayo kuna wasomi kushinda wao katika ngazi za uongozi wa chini?

Ni rahisi kuelewa kwa nini hakuna anayetaka kugombea nafasi za kuwa mjumbe wa nyumba kumi au balozi au diwani au mwenyekiti wa serikali ya mtaa. Kwa upande mwingine kila mtu anataka kugombea ubunge, uwakilishi na urais. Hata hao waliopo asilimia 80 ya muda wao hutumika kujitafutia riziki kwingineko na ni kama asilimia 20 tu ndiyo hutumika kuangalia mambo ya wananchi/serikali.

Kutokana na ukweli huu kwamba kuna mfumo na hali ambayo inasababisha watu watake kugombea ubunge, uwakilishi na urais, lakini hakuna wanaotaka kugombea ubalozi au uenyekiti wa mtaa. Ni dhahiri kuwa ipo haja ya kuleta mapinduzi makubwa ya uongozi katika ngazi za chini ikiwa kama kweli tunataka tujikwamue na hali hii ya kuwa masikini wakubwa duniani. Na uongozi wowote (uwe wa chini au wa juu) lazima uwe ni kazi au tarafu inayolipwa kima mahsusi kinachowawezesha viongozi hao wote kujitoa kwa hali na mali kutimiza zaidi majukumu yao ya kikazi kuliko ya kibinafsi.

Tuanze na utafiti na ushauri

Ninapendekeza kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kikishirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania chenye tawi karika kila mkoa waanze kwa utafiti na ushauri katika kuona ni namna gani tunaweza kuongeza hatua kwa hatua, ubora wa viongozi waliopo na wakati huo huo kuwashawishi watu wenye uwezo, elimu na ujuzi zaidi kukubali kuwa wajumbe wa nyumba kumi na viongozi wa serikali za mitaa. Bila kuwasahau madiwani wetu. Baada ya kazi za utafiti na ushauri yaanze mafunzo na uandaaji wa mipango ya urithishaji uongozi kwa namna ambayo kila mtaa, kila kata inapata kiongozi anayestahili kushika nafasi hiyo.

Ninaamini kwamba, masomo kama ya uchumi, uongozi,utawala, uangalizi wa fedha, menejimenti, sayansi ya jamii, usimamizi rasilimali watu, mipango, udhibiti, sayansi ya maamuzi na kadhalika hayatakosekana na yatatolewa kwa lugha mama ya Watanzania, yaani, Kiswahili.