Tuesday, April 23, 2013
Migogoro ya Kiimani matunda ya kukosa uongozi jumuishi, bora na adilifu kijamii, kiuchumi, kidini na kisiasa
NCHI zote ambazo asili na utu wao unatawakali mbele ya vitu vingine duniani ndizo zilizotulia na zilizoepuka machafuko na migogoro ya kijamii na kiimani kwa kiasi kikubwa. Kuanzia Uarabuni, Uchina, India, Urussi, Vietnam, Malaysia, Indonedia, Ufilipino na kddhalika.
Matatizo katika nchi hizi yanakuja pale mataifa haya yanapoanza kuzainiwa na kuacha kutanguliza asili, historia na utu wao kwanza na wakakubali kutanguliza kitu kingine mbele iwe dini au maslahi fulani au ukabila au ueneokijiografia au uchama na kadhalika.
Utaifa, historia, desturi na utamaduni wa watu vinapopewa hadhi stahilifu husaidia sana na kuiepusha nchi kukwepa pepo za ushawishi na mbadaliko ya kimtazamo kutokana na kuingiliana na watu wa asili na tamaduni nyingine.
Migogoro ya kiimani Afrika na hususan Tanzania ni matunda ya kuurudisha nyuma Utanzania na Uafrika wetu na kutanguliza maslahi ya kiitikadi na kibinafsi miongoni mwetu na hasa kati ya viongozi wetu.
Hili nalo kwa maoni yangu linasababishwa na kushindwa kutambua kwamba uongozi bora ni jambo la ushirika kiushauri na la pamoja. Ukijenga ukiritimba katika uongozi mara nyingi unaharibu, badala ya kutengeneza.
Kila jamii ina aina mbalimbali ya viongozi. Kuna viongozi wa kiseriikali, kisiasa, kiimani, kimila/kiutamaduni, kiuchumi/kibiashara, kiteknolojia na kadhalika. Pale viongozi wa kiutawala au wa kisiasa wanapoona kwamba wao ndio tu wanaostahili kuitawala jamii na sio viongozi wa aina nyingine, basi migogoro katika jamii hiyo haiishi na imani ya wananchi kwa viongozi wao hao hupungua kwa kiasi kikubwa.
Katika hili yapo mengi ya kumuiga mwasisi wa taifa hili, Mwalimu J.K. Nyerere na moja kubwa ni kwamba hakusita kuwaita na kuwaambia waziwazi na bayana viongozi wa kiimaniya kwamba mpaka we0katika hili ni huu hapa na msivuke mstari huu. Maana Mwalimu aliutanguliza kwanza Uafrika na Utanzania wake kabla ya kitu kingine. Kuutanguliza Utanzania, Uafrika na utu wetu mbele ya kttu kingine ndiyo nguzo ya kwanza ya amani na umoja wetu. Athubutu mwingine kutwambia vingine. Ninaona katika hili, hivi leo kuna udhaifu mkubwa miongoni mwa viongozi wetu.
Endapo tunataka kuondokana na migogoro inayolinyemelea taifa letu kwa hivi sasa ni lazima tuukubali ukweli huu hapo juu na kuanza kuandaa mifumo na miundo ambayo itawapa viongozi wote katika sehemu na ngazi zote nafasi ya kuchangia maendeleo ya nchi na watu wetu.
Kinachoonekana kwa hivi sasa ni kwa viongozi wetu mbalimbali kuchomwa moyo zaidi na kujihusisha na vidonda na vipele na sio chanzo halisi cha gonjwa la kukosa sio tu amani bali upendo, ushirikiano na kuaminiana kati ya wanacnhi wetu kama ilivyokuwa kwenye awamu ya kwanza ya serikali ya Tanzania.
Ieleweke hakuna Mtanzania mmoja aliyekuwa na akili kuliko Watanzania wote wakiwekwa pamoja na anayeamini hivyo sio tu anajidanganya ila yeye ni tatizo kubwa. Akili ni nywele na kila mtu ana zake.
Taaluma, uwezo na kushindwa kujifunza kutokana na historia na watu wengine kwa ujumla ninaamini ni jambo moja linalochangia kuwepo kwa migogoro ya kiimani ambayo isingelikuwepo kwenye miaka ya sabini na themanini hapa nchini kutokana na dini kuwa mikononi mwa viongozi walioisoma jamii vyena ma waliojitahidi kutoa mchango wao katika kuifanya jamii yetu kuwa kitu kimoja.
Hizo ni enzi ninazozikumbuka wakati wa viongozi kama Hemedi bin Juma, Kadinali Rugambwa, Askofu Moshi, Askofu Sangu na viongozi wa dini nyingine ndogo kwa kubwa waliojua kutenga kilichokua cha Kaizari na kilichokuwa cha Mungu. Leo tuna mamia ya watu wanajiona wao ni bora mara mia ya viongozi wao. Lakini tukumbuke pamoja na yote uongozi ni zawadi kwa wema au ubaya toka Kwa Mungu.
Katika miaka hii kwa bahati mbaya sana kila sekta inaingiliwa na wanasiasa, matajiri na watu kama hao wanaotaka kuwatumia watu wengine kujitajirisha, kujenga umaarufu na wakati mwingine kuihadaa na kuigombanisha jamii kwa maslahi yao binafsi na sio maslahi ya walio wengi. Izingatiwe kwamba katika taifa lolote kuna asilimia ya watu 97 wanaofikiri kwa moyo na ni asilimia chini ya 3 wanaofikiri kwa akili. Ni asilimia hii 3 ndiyo ambayo aghalabu inayozusha matatizo ya kila aina. Huwa wanadhani wanajua, kumbe hawajui kitu. Wanajihadaa wao wenyewe na wale wanaowahadaa kwa hasara ya nchi na watu wake.
Ipo haja ya kuwa na Taasisi ya Kuwafunza viongozi wote wawe wa kisiasa au kidini au kibiashara mahala pamoja juu ya nadharia na dhana na imani na kanuni za msingi zitakazochangia kutuunganisha badala ya kutugawa. Kwa namna hii, kila kiongozi nchini wa kundi lolote lile atajifunza lililo sawa kufanza na lisilo sawa kulifanza pale anapoteta au kufanya jambo lolote lile hadharani.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingelipitia kwa mara nyingine tena uwepo wa 'World Conference of Religions for Peace' hapa nchini (taasisi muhimu sana inayopuuzwa kiasi cha kutisha) na kuona ni kwa namna taasisi hiyo inaweza kushikishwa na kuwezeshwa kufikia malengo na madhumuni yake ambayo kwa mapana na marefu ni hayo hayo au pengine zaidi ya hayo aliyogusia na anayoyahofia mheshimiwa Kikwete katika hotuba yake ya hivi karibuni.
Kinachoonekana hapa nchini ni kwamba kuna watu na taasisi kabakaba ambazo zikiachwa kupuuzwa na zikashirikishwa katika changamoto na vilio vyetu mbalimbali vya kila siku, taasisi na watu hao wanaweza kutoa mchango wenye thamani na faida kubwa kwa nchi na watu wetu. Tuzinduaneni na tufanye kweli, lawana na hotuba zisizokwisha na zisizobadili kitu haziwezi kutufaa kwa lolote.
Kisiasa ni muhimu kupitia upya na sera zinapendelea wanachama wa chama fulani na kubagua wa vyama vingine. Wanasiasa wakifanya hivyo, je, watu wa Mungu nao watahesabika wamefanya kosa na wao wakifanya ubaguzi kama huo? Wanasiasa wetu waelewe kuwa demokrasia na mfumo kamili, unapouwekea vikwazo upande mmoja, unachangia pia kuvuruga na kwignine usikokujua.
Unafiiki na undumilakuwili ambao aghalabu unachangia mara kwa mara isijulikane kama hivi leo wanasiasa hapawanasema kweli au uongo hauwezi kutusaidia katika changamoto zilizo mbele yetu. Lazima viongozi wa dini na kisiasa wakubaliane kwamba nchi yetu haiwezi kujengwa juu ya misingi ya uongo, Kujitia uziwi na upofu unapoambiwa kweli, ubinafsi, kufikiri kwa moyo badala ya akili, kujigeuza kifaurongo, uzushi, kupakazina, umbeya, hadaa na uzaini wa kidizaini na kisanii bali katika misingi ya ukweli, uwazi, haki, usawa wa kisheria na uwajibikaji na vinginevyo ni kujidanganya kwa hasara ya walio wengi.
Kwa kuanzia nawatafadhalisha viongozi wetu wote kujua ni mahala gani au wapi pa kusema yanayowahusu viongozi na wapi pa kumwaga mtama mbele ya kuku au bata wote.
Ikiwa hivi tutakuwa na viongozi ambao mikono yao inafungwa na mikono ya viongozi wengine nchini na inakuwa ni rahisi kuwafuatilia na kuwadhibiti wanakosea na kuwatoa kwenye kundi la uongozi.
Hatua hii italiepushia taifa madhara kama tunayoyaona kwingine Afrika. Mimi kama mwananchi wa kawaida nawatafadhalisha viongozi wetu kabla hawajafungua mdomo kutuambia chochote basi wazungumze wenyewe kwa wenyewe kwanza, wapime na kutathmini nini itakuwa atahri yake wanacnhi watakapofafanuliwa jambo hilo.
Hatari kubwa ninayoiona kwa amani na umoja wa Tanzania sio kitu kingine ila midomo na kauli za viongozi wetu (kwa maana hiyo pana), kwamba kipo watakachokisema kitakachotuleta madhara makubwa kama ilivyo kwa watakachoacha kukisema nacho kikatuleta shari kubwa pia. Ninaamini viongozi wote kwa pamoja wana dhamana ya kulizungumzia hili na kujifunza kutoka kwa wengine itifakizinazoendana na matamshi yanayogusa sehemu kubwa ya watu wetu au taifa kwa ujumla wake. Viongozi wanapokuwa kitu kimoja katika kuongoza wale wanaostahili kuongozwa wana uwezo mkubwa zaidi wa kujenga amani na umoja kuliko vinginevyo. Mungu ibariki imani zetu, Mungu tubariki Tanzania na Afrika na tujalie kuutanguliza Utanzania na
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment